Na Fatma
Amir
ALIYEKUWA
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck
Sadiki, amefunguka kwa kusema moja ya changamoto aliyokumbana nayo wakati akiwa Dar es Salaam,
ni vuguvugu la uchaguzi mkuu la mwaka 2010.
Uchaguzi huo
ulihusisha wagombea wa vyama vyote wakiwemo Rais Mstaafu Dk. Jakaya Kikwete wa
Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Dk. Wilbroad Slaa aliyegombea kwa tiketi ya chama
cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Sadiki
ambaye sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro aliyasema hayo jana jijini Dar es
Salaam katika sherehe ya kuagwa iliyohusisha viongozi wa dini wa kiislam na
Kikristo.
Aidha,
aliwaomba viongozi wa dini wamuunge mkono Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul
Makonda, katika kampeni ya ‘kusafisha jiji ondoa uchafu’.
“Wananchi wa
Dar es Salaam ndio wamenifikisha hapa nilipo,
hadi Rais Magufuli alipoamua
kunipeleka Mkoa wa Kilimanjaro kwenda
kuendeleza mazuri niliyoyafanya hapa,” alisema
Aidha,
aliwaomba viongozi wa dini kuendelea kumwombea ili akafanye kazi kama
alivyokuwa akiifanya alipokuwa Dar es Salaam.
“Nikuombea
Makondaufanye kazi pamoja na kamati ya
viongozi wa dini uwashirikishe changamoto utakazokumbana nazo ili wakusaidie
katika kukuombea,” alisema.
Makonda
aliendelea kusisitiza kuhusu mpango aliopanga kuanza nao wa kuondoa gereji
zilizopo mitaani, baana yadi za magari zihamie maeneo maalum lengo likiwa ni
kuifanya Dar es Salaam kuwa safi.
“Uchafu unaanzia moyoni mwako, nawaomba
wananchi kila mmoja asafishe maeneo yao,” alisema.
Aidha,
amewataka viongozi wa Serikali ya Mtaa wampatie idadi ya wananchi wanaoishi
eneo yao ili ulinzi uweze kuimarishwa.
“Nashukuru
Rais John Magufuli kwa kunichagua kufanya nae kazi, namshukuru baba yangu Meck
Sadiki leo ni siku iliyofungua kurasa
mpya ambayo sikuwahi kuusoma,”alisema
Kwa upande
wake aliyekuwa mgeni rasmi Mbunge wa
Bunge la Afrika Mashariki Abdula Ally Hasani Mwinyi alisema kwa upande wake hana tatizo na uongozi wa Paul Mkaonda yeye ni kiongozi bora.
“Matatizo
yakukosa amani yana vyanzo vingi ikiwemo dini, wananchi kukosa kipato, uhaba wa
risilimali na hayo ndio yanayodumaza maendeleo ya taifa.”alisema Mwinyi
Mwinyi
alimtaka Makonda kuwa msikivu kwa viongozi wa dini na viongozi wengine ili kuwa
kiongozi bora.
Mwisho

0 comments:
Post a Comment