Mnigeria mmoja ameuliwa na rafiki yake huko Mumbai juzi jumamosi usiku kufuatia kubishana nani mchezaji bora kati ya Cristiano Ronaldo na Lionel Messi
Kwa maelezo ya Polisi, Obina Michael Durumchukwa,34,alikuwa anasheherekea siku yake ya kuzaliwa akiwa na rafiki yake Nwabu Chukwuma,22, na baadaye wakaingia katika ubishi huo wa nyota hao wawili.
Polisi huyo, Kiran Kabadi amesema kuwa,Durumchukwa alianza kurusha glasi kwa Chukwuma, akamkosa na kugonga ukutani, Chukwuma akachukua vile vipande vya glasi na kurusha, vikamchana Durumchukwa kwenye koromeo
Baada ya tukio hilo Chukwuma amekamatwa na Polisi kwa kosa la Mauaji. .

0 comments:
Post a Comment