
Amanda Laswai
"Panya alimeza kipande cha dhahabu mwenye dhahabu akachanganyikiwa na kuamua kumkodi mpelelezi mmoja ili aje amuue panya aliyemeza dhahabu.
Mpelelezi alipofika alikuta panya zaidi ya 500 lakini alishangaa kumuona panya mmoja kajitenga,ndipo alipomkamata na kumuua,alipompasua akakuta kipande cha dhahabu akamkabidhi mwenyewe.Yule jamaa akashtuka huyu mpelelezi alimjuaje yule panya ikabidi amuulize.Jamaa:bwana we mkali,ulijuaje kama huyu ndiye panya aliyemeza dhahabu?
Mpelelezi:hawa panya nao ni kama baadhi ya raia waafrica wakiwa na mali kidogo hujitenga na wenzao"

0 comments:
Post a Comment