Hujafanikiwa bado kama huna uwezo wa kumweka mtu mwingine mjini. Hujafanikiwa bado kama hujaanza kutengeneza ajira kwa vijana wenzako.
Kwa wengi, bado wanategemea kuajiriwa lakini kwa wale waliojituma, leo hii wametoka kwenye kuajiriwa na sasa wao ndio wanaoajiri, Vanessa Mdee ni mmoja wao.
Miaka mitatu minne iliyopita, Vee Money alikuwa mwajiriwa kama vijana wengine. Alitegemea mshahara kutoka kwenye kazi yake ya utangazaji wa TV kwenye kituo cha MTV Base na Choice FM. Kwa wengi, waliamini kuwa kipato alichokipata kwenye kazi hizi mbili nzuri kilimtosha kutimiza kila kitu alichotaka.
Lahashaa, Vee alitaka makubwa zaidi na ndio maana aliifufua career yake ya muziki ambayo mwanzo wakati anaanza, wengi walikuwa na mashaka naye. Ni kwasababu, ni watangazaji wachache walioingia kwenye muziki na wakafanikiwa. Vee alikuwa determined, ndio maana baada ya kuona kuwa hawezi kutumikia mabwana wawili, aliamua kuacha utangazaji na kuanza kufanya muziki kwwa 100%.
Huo ulikuwa ni uamuzi bora kuwahi kuufanya kwenye maisha yake. Leo hii Vee ni msanii namba moja Afrika Mashariki. Ana show kibao, ndani na nje ya nchi. Na sasa amefikia yale mafanikio ambayo nimeyasema kwenye aya za mwanzo, kuweza kutoa ajira kwa wengine.
“Mungu ni mwema sana eti leo na mimi natoa ajira. Dah! #NeverEver give up #ComeDanceWithVee #VeeMoneyDanceAuditions,” aliandika Vanessa.
Mamia ya vijana Dar es Salaam walijitokeza kwenye usaili wa kuwa dancers wa Vanessa
Muimbaji huyo alifanya usaili wa kutafuta dancers watakaokuwa chini ya label yake, Mdee Music. Inamaanisha kuwa, dancers hawa watapata ajira kupitia vipaji vyao. Hongera Vanessa kwa kutumia kipaji chako kutoa ajira kwa vijana wenzako.


0 comments:
Post a Comment