Sunday, April 24, 2016

ZUWENA MOHAMED ‘SHILOLE’Alianzia kwenye filamu kisha akajiingiza kwenye muziki. Kwa mujibu 
wake mwenyewe, aliwahi kukiri kuwa aliingia kwenye fani hizo kwa 
ajili ya kujitafutia kipato ili kulea wanaye. Aliolewa ndoa ya kwanza 
huko kwao Tabora na kuzalishwa mtoto mmoja kisha ndoa ikaota
 mbawa. Hakukaa muda mrefu akapata mwanaume mwingine
 ambaye alimpa ujauzito na kuzaa mtoto wa pili. Aliwahi kusema 
kati ya wanaume hao, hakuna anayemsaidia kulea.

MIRIAM JOLWA ‘JINI KABULA’Alianzia kwenye uigizaji kisha urembo na sasa ameongezea muziki.
 Amezaa na Mkurugenzi wa Tuesday Entertainment, Tuesday 


Kihangala ‘Mr Chuz’ ambapo walijaliwa kupata mtoto mmoja wa 
kike na baada ya hapo mapenzi yakaisha. Kwa kuwa mapenzi
 yalikwisha, Jini Kabula alibaki na mwanaye akimlea 
mwenyewe japo Mr Chuz huwa anampiga ‘tafu’.

SNURA MUSHI Alianzia kwenye uigizaji kabla ya hivi karibuni kujikita pia katika tasnia
 ya filamu. Ana mtoto mmoja wa kike. Anakiri kuwa tangu akiwa mjamzito
 baba mtoto wake aliingia mitini. Mpaka sasa anamlea mwanaye
mwenyewe kupitia sanaa ya filamu na muziki.

MAUNDA ZORROAlipata umaarufu kupitia muziki na baadaye akaongezea uigizaji. 
Ana mtoto mmoja na huwa hapendi kumwanika mwanaume 
aliyemzalisha ambapo mpaka sasa anaishi nyumbani kwa baba yake, 
mzee Zahir Zorro na hakuna dalili zozote za ndoa.

1 comment:

  1. Rekebisha kichwa cha habari,sio kwamba baba za watoto hawafahamiki ni hawatoi matunzo.Mnakaa kucheka wanaochapia English lugha ya wary na nyie mnaochapia lugha yenu ni nani kati yenu wa kuchekwa?

    ReplyDelete