Meneja wa Tip Top na WCB, Hamisi ‘Babu Tale’ Tale tale, amewataka wasanii wa muziki Tanzania kufanya kazi kwa bidii ili kuendana na mabadiliko makubwa katika tasnia ya muziki hivi sasa.
Babu Tale amedai wasanii wengi wanashindwa kuendana na kasi ya mabadiliko haya, na ndio maana mara kadhaa wanalalamika ‘kubaniwa’.
“Game sasa hivi imebadilika imekuwa ngumu, usipoangalia utamtukana kila mtu kwamba unabaniwa sijui nini,wapo watu wana shine bila uongozi na watu hawashine bila uongozi.
“Game imebadilika sana inafanya vitu inavyotaka yenyewe, ukiweza kujua watu wanataka nini ndio utaendelea kuwepo” Alisema.
0 comments:
Post a Comment