Tuesday, April 5, 2016

085A9790
Polisi wakichukua mwili wa marehemu kwa ajili ya uchunguzi.
Mfanyabiashara raia wa China aliyetambulika kwa jina la Luo Dongpeng (32), maiti yake imekutwa ndani ya gari lenye namba za usajili T145 DFY Machi 28, mwaka huu maeneo ya Kijitonyama, Wilaya ya Kinondoni jijini Dar,Uwazi linakupasha.

1
Gari aina ya Nissan X-Trial alimokutwa amenyongwa mchina huyo.
Taarifa zilizopatikana kutoka kwa mashuhuda wa tukio hilo wanaoishi  maeneo aliyokutwa Mchina huyo zinaeleza kuwa, gari la marehemu huyo walianza kuliona hapo tangu alfajiri ya siku hiyo lakini kadiri muda ulivyokuwa ukienda ndivyo walivyozidi kulitilia shaka maana hakukuwa na mtu aliyetoka ama kuingia.
Waliendelea kusema kwamba ilipofika saa 10.00 jioni walilazimika kulisogelea na kuchungulia ndani ndipo walipomuona mtu akiwa amelala kiti cha nyuma, walipomwamsha hakuamka wala kujigeuza ndipo waliwaarifu polisi wa Kituo cha Mabatini Kijitonyama.
085A9757
Moja ya msumali uliokuwa umetegwa kwenye gari hilo.
Mashuhuda hao walidai kuwa huenda Mchini huyo aliuawa kisha kutelekezwa na gari lake maeneo hayo kwani alikuwa na michubuko mikononi na shingoni.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, ACP Alphonce Fuime alipohojiwa na gazeti hili wiki iliyopita ofisini kwake alikiri kutokea kwa mauaji hayo.

0 comments:

Post a Comment