MUSA MATEJA, amani
DAR ES SALAAM: Wakati msuguano mkubwa ukiwa umeibuka, Mbongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’ akisukuma madongo kwa Magazeti Pendwa ya Global Publishers kwamba yanamtungia uongo kuhusu hali yake ya kurejea kubwia unga akisema hayuko hivyo kwa sasa, kuna taarifa kwamba, Rais Mstaafu, Jakaya Mrisho Kikwete ‘JK’ amemuonya kuhusu kutozingatia matumizi ya dawa za methadone.

Methadone
ni dawa zinazotumiwa na waathirika wa matumizi ya madawa ya kulevya
‘unga’ ambapo Ray C anatumia kwenye Hospitali ya Mwananyamala, Dar baada
ya kuathirika.
Kwa
mujibu wa chanzo chetu makini hospitalini hapo, Ray C alipata onyo hilo
baada ya Magazeti ya Global kuandika kwamba nyota huyo amerejea kwenye
kubwia unga huku akiendelea na methadone, hali ‘inayomzimisha’ mara kwa
mara.
“Jamani
nataka kuwaambia, mnajua mlipoandika kwamba Ray C karejea kwenye unga
wakati akiendelea kutumia methadone, JK alisoma, akamtumia ujumbe
akimtaka ajiangalie kwenye kukazana kutumia dawa na kuachana moja kwa
moja na matumizi ya unga.
“JK amemtaka aangalie mwenendo wake kwa sasa. Yaani bwana sijui vipi, JK anamtakia mema lakini yeye hajijui tu.
“Lakini kubwa kuliko yote ni kwamba juzikati Ray C alikuja pale Hospitali ya Mwananyamala (jijini Dar), akawaangukia madaktari wake wanaomtibu akiwaomba msamaha kwamba amekuwa akiwapuuza katika ushauri lakini amegundua wao ndiyo msaada mkubwa kwake,” kilisema chanzo hicho.

Kitendo
hicho kinatokana na madaktari hao siku za karibuni kumshindwa staa huyo
katika kumpa mwongozo wa matumizi ya dawa hizo, hivyo kuamua kumrudisha
nyumbani kwao, Bunju, Dar (habari hiyo iliandikwa na gazeti hili).
Taarifa zaidi zinasema kuwa pia baada ya Magazeti ya Global kuandika habari ya anayemmaliza Ray C ni kijana Frank, ndugu zake wamemfuata na kumrudisha nyumbani kwao, Arusha.

“Unajua ndugu zake walikuwa wakimtafuta, alipotoka kwenye gazeti wakamwona, wakamfuata Mwananyamala kumchukua,” kilisema chanzo.
Utafiti
uliofanywa na gazeti hili, umebaini kuwa ile ‘posti’ ya Ray C
aliyoitupia kwenye mtandao wake wa Instagram mara baada ya kuandikwa na
Gazeti la Ijumaa Wikienda la Machi 28, mwaka huu, habari ikiwa na
kichwa; RAY C ANASWA AMEZIMIKA, akitoa shutuma nzito kwamba picha zile
si zake bali ziliungwaungwa, ameifuta!
Udadisi zaidi unasema kuwa kufutwa kwa posti hiyo kunatokana na Mbongo Fleva huyo kuguswa na dhamira yake huku pia michango ya wafuasi wake waliojitokeza kumwandikia ukweli kumwambia, picha zile ni yeye na hakuna aliyeziunga!
Ray C alipotafutwa juzi ili kujibu madai hayo alikosekana hewani licha ya kupigiwa simu mara kwa mara kwa siku nzima.

0 comments:
Post a Comment