Watoto
watatu kutoka kijiji cha Barca katika kaunti ndogo ya Aber Wilayani
Oyam nchini Uganda wameanza kuzungumza lugha tofauti isiojulikana baada
ya kufungiwa katika nyumba kwa miaka saba.Lugha hiyo mpya imetajwa kuwa
Leb -adam ikimaanisha lugha ya ubongo na jamii ya eneo
hilo.Inadaiwa kuwa baba ya watoto hao aliwafungia ili kuwalinda kutokana na hatari yoyote.
hilo.Inadaiwa kuwa baba ya watoto hao aliwafungia ili kuwalinda kutokana na hatari yoyote.
Kulingana
ma gazeti la the monitor nchini Uganda,watoto hao hawajaathirika
kiakili lakini hawawezi kuzungumza na watu wengine.Wanaamini tu kile
baba yao anachowaambia.
Kulingana na mama yao watoto hao
waliweza kuishi kwa kula mayai ya chura yaliochemshwa na majani,ambayo
hula kila asubuhi na jioni na hutumia maji kutoka shimo lililochimbwa na
baba yao.
Mama yao anasema kuwa baba ya
watoto hao alimzuia kutozungumza nao hatua iliowafanya kutojifunza lugha
ya kiluo wakati walipokuwa wadogo.
Mwanamke huyo amesema kuwa alionywa na baba huyo kutosema chochote kuhusu watoto hao.via>>BBC
0 comments:
Post a Comment