Msanii wa bongo fleva Nay wa Mitego ambaye kwa sasa anafanya poa na kazi yake mpya 'Shika Adabu Yako' amefunguka na kuonesha hisia zake kwenye kazi mpya ya msanii kutoka Kenya Khaligraph Jones ambayo inaitwa 'Mazishi'.
Nay wa Mitego baada ya kuisikiliza kazi hiyo ya Khaligraph Jones alisema kuwa katika watu ambao ni ma-rapa wazuri na wanachana sana basi huwezi kushindwa kumtaja rapa Khaligraph Jones kutoka Kenya na kudai mwana ni mkali kupitiliza.
"Wanajua ni 'Mazishi' by Khaligraph Jones toka Kenya. Kama kuna ma-rapa wanachana mmmmh huyu jamaa anavunja daming. Hii ngoma ni kali sana" alindika Nay wa Mitego kwenye Acount yake ya Instgram.
Mashabiki wa Nay wa Mitego waliungana naye na kusema kuwa wimbo huo wa Khaligraph Jones ni wimbo ambao uko poa sana na kwamba jamaa ameonesha uwezo mkali huku wengine wakimwambia Nay wa Mitego kuwa hata yeye kwa mwana hawezi kusogea na kudai kama anabisha ajaribu kumdiss aone uwezo wa Khaligraph Jones katika diss.
0 comments:
Post a Comment