Thursday, April 21, 2016


Msanii chipukizi wa bongo fleva Bright ambaye amekuja na wimbo wake wa Nitunzie aliomshirikisha Baraka Da Prince, aamefunguka hisia zake juu ya diva wa bongo fleva vanessa Mdee, huku akitangaza vita na Jux

Akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa radio, Bright anasema ana ndoto kubwa ya kumuoa diva huyo ambaye ni mwandani wa msanii Jux, huku akiweka wazi kuwa Jux hamuogopi kwani hajamuoa.
“Nampenda sana natamani kumuoa ndoa kabisa, unajua msicheke ni kitu ambacho naongea niko serious kabisa, natamani kumuoa kabisaa, ni mwanamke mzuri mwenye mvuto, mwanaume yoyote aliyekamilika lazima atamani”, alisema Bright.
Mtangazaji wa kipindi hiko Dulla alipomuuliza kuhusu itakuwaje iwapo Jux akijua, alijibu kwa kujiamini kuwa hana wasi wasi kwani Jux hajamuoa Vanessa, na yeye anataka kumuoa kabisa awe mke wake wa ndoa,
“Niko kwenye process hata kama Jux yupo naye, hawajaoana nina nafasi ya kumwambia nikamvisha pete ndoa kabisa, na sio namsubiri amuache, naweza nikamnyang'anya braza, mpaka sasa hakuna aliyetangaza ndoa kwa V Money”, alisema Bright.
Pamoja na hayo yote Bright amesema wimbo huo anau-dedicate kwa Vanessa, akimtaka amtunzie ili amuoe, huku akiwataka mashabiki kumuunga mkono kwa kuomba nyimbo yake ipigwe kwenye radio.
Sikiliza Wimbo wa Bright ft Baraka da Prince - Nitunzie hapa.

0 comments:

Post a Comment