Mkuu wa Mkoa wa Mbeya amewataka wenyeviti , watendaji wa Vijiji na kata wilaya ya mbarali kutouza ardhi ovyo pasipo kuzingatia taratibu na sheria ya ardhi kinyume na hivyo atawachukulia hatua Kali
Amesema pamoja na sheria kuwapa Mamlaka kabla ya kugawa ardhi kwa wawekezaji waangalie mahitaji ya kijiji kwanza kwasasa na siku zijazo
Ameagiza uongozi wa wilaya kusimamia Vijiji kuwa na matumizi bora ya ardhi ili kuondoa migogoro ya wakulima na wafugaji
Amelitaka jeshi la polisi, Kamati ya Ulinzi na usalama kushirikiana na wananchi kuchukua hatua za haraka kuepusha migogoro ya wakulima na wafugaji na uvunjifu wa amani






0 comments:
Post a Comment