Posted by Williammalecela.com on Thursday, April 21, 2016
 |
MKUU wa mkoa wa
Mbeya Amos Makalla ameunda kikosi kazi cha watu 14 kilichogawanyika
katika makundi mawili ambacho kitapitia upya uhakiki wa majina ya
watumishi hewa na kurejea kufanya uhakiki kati ya April 20 hadi 24.
Makalla aliagiza uhakiki huo kufanyika kati ya tarehe 25 hadi 29 ambapo
awali alipata taarifa ongezeko la watumishi hewa 3 katika halmashauri
ya Jiji la Mbeya na watumishi 7 kutoka halmashauri ya Mbeya.
Alisema katika uhakiki wa awali Mkoa wa Mbeya na Songwe uligungulika
kuwa na watumishi hewa 94 waliosababisha hasara ya sh milioni 457 na
kuwa hadi sasa kuna jumla ya watumishi hewa 10 kati ya watumishi hewa
saba ambapo Halmashauri ya Mbeya ina jumla ya watumishi 23 kutoka
watumishi hewa 16 waliotajwa awali.
Makalla amewataka wafanyakazi
wote kufika mbele ya kamati wakiwa na barua ya mwajiri, vitambulisho na
Payroll ya mwezi Machi 2016 na kuiagiza kamati mara baada ya kufanya
uhakiki watakaobainika na kesi za kujibu waburuzwe mahakamani na
kutakiwa kurejesha fedha zote za serikali.
|

0 comments:
Post a Comment