Saturday, April 2, 2016

page
Msanii wa muziki nchini Amini ameweka wazi ujio wa kazi yake mpya aliyoshirikiana na msanii wa Nigeria Selebobo.

Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na video yake mpya ya wimbo Hawajui, amekiambia kipindi cha Siz Kitaa cha Clouds TV Jumanne hii, kuwa kolabo yake na Selebobo tayari imekamilika.
“Kolabo zinakuja nyingi tu mashabiki wangu wasiwe na haraka, tayari nimefanya kazi na Selebobo wa Nigeria, nilimtumia kazi na yeye akafanya, tena ndani ya siku tatu akawa amekamilisha nilichomwambia, kwa hiyo kazi ipo tayari mashabiki wasubirie muda ukifika itatoka,” alisema Amini.
Pia Amini alisema yupo kwenye harakati za kufanya kolabo nyingi zaidi ili na yeye kujiweka vizuri kimataifa.

CHANZO na Bongo5


0 comments:

Post a Comment