Meneja wa wasanii Babu Tale amefunguka juu ya 'bifu' linaloendela kati yake na msanii Baghdad, ambalo limepelekea kwa sasa kutolewa wenye group la whatsapp la wasanii.
Akizungumza kwenye kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa Radio, Babu Tale amesema kuhusu suala hilo kama Baghdad anatafuta promo ya kazi zake mpya, hiyo sio njia sahihi na badala yake amfuate ili ampe kiki.
“Sitaki kumpa promo hiyo, akitaka promo aje nimpe promo sio hiyo”, alisema babu Tale.
Pia Babu Tale amekiri kutolewa kwenye group hilo, na kusema kuwa kabla yeye hajatolewa alishawatoa wasanii wote ambao anawasimamia na kisha yeye akatolewa.
“Mimi nimewatoa watu wangu, wasanii wangu wote ambao nawasimamia mimi alafu baadaye wasanii ndo wakanitoa”, alisema Babu Tale.
Sauti ya Babu Tale akiongelea ishu ugomvi wake na Baghdad.
0 comments:
Post a Comment