Saturday, April 16, 2016

MagufuliRais Dkt. John Pombe Magufuli (kulia) pamoja na Balozi wa Japan nchini Tanzania Masaharu Yoshida (kushoto) wakiweka jiwe la msingi kama ishara ya kuzindua rasmi Mradi wa Ujenzi wa Barabara ya Flyover -Tazara huku wakishuhudiwa na viongozi mbalimbali wa serikali.MagufuliqRais Dkt. John Pombe Magufuli na Balozi wa Japan nchini Tanzania Masaharu Yoshida wakikata utepe kama ishara ya kuzindua rasmi mitambo itakayotumika katika ujenzi wa Mradi wa Barabara ya Flyover -Tazara huku wakishuhudiwa na viongozi mbalimbali wa serikali.
FLY Over (3)Wakandarasi watakaojenga daraja hilo.FLY Over (1)FLY Over (2)Kikundi cha ngoma wakitoa burudani za utangulizi.
FLY Over (4)Jukwaa kuu.FLY Over (5)Wageni waliohudhuria hafla hiyo wakichukua nafasi zao na kuketi.

FLY Over (6)Brass Bendi ya Polisi wakitumbuiza.FLY Over (7)
Mbunge wa Ilala, Mussa Azan ZunguFLY Over (8)
Wakisalimiana.
HII ni taswira ya maandalizi ya uzinduzi wa mradi wa ujenzi wa barabara za juu (Fly Over) katika makutano ya barabara Nyerere na Mandela (Flyover ya TAZARA) jijini Dar es Salaam ambapo Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amezindua rasmi mradi huo leo Jumamosi tarehe 16 Aprili, 2016.
Flyover ya Tazara, Dar itakuwa ni barabara ya pili kwa ukubwa Afrika Mashariki baada ya Super High Way ya Kenya iliyozinduliwa mwaka 2012 iliyojengwa kwa Ushirikiano wa Benki ya Afrika na Serikali ya Kenya.
Aidha mradi wa ujenzi wa barabara za juu Flyover ya Tazara unatarajiwa kukamilika ifikapo Oktoba 2018 hivy kupunguza adha ya msongamano kwenye barabara hiyo kwa asilimia 80.

0 comments:

Post a Comment