Boniphace Ngumije na Mayasa Mariwata, RISASI
DAR
ES SALAAM: Wakati wadau wa muziki wakifahamu kuwa Msanii wa Muziki wa
Hip Hop Bongo, Rashid Makwilo ‘Chid Benz’ yuko katika kituo cha kusaidia
waathirika wa madawa ya kulevya ‘sober house’ kilichopo Bagamoyo mkoani
Pwani, inadaiwa jamaa alishatoroka kitambo na sasa yuko kitaa.
Taarifa
iliyotua kwenye meza ya dawati hili ilidai kuwa, Chid alitoroka kituoni
hapo baada ya kushindwa kuhimili mazingira yalikuwepo hivyo akaona bora
arudi mtaani kwa staili ya liwalo na liwe.
Baada
ya kupata taarifa hiyo, mwishoni mwa wiki iliyopita waandishi wetu
walitinga Bagamoyo na kukutana na meneja wa kituo hicho, Tumaini Majura
ambaye alithibitisha kuondoka kwa Chid akiwa bado anaendelea kupatiwa
matibabu. Sehemu ya mahojiano kati ya Risasi na meneja huyo ni hii;
Tumaini: Ni siku 28 lakini alitakiwa kukaa kwa muda wa angalau miezi mitatu ili kurudi katika hali yake ya kawaida.
Risasi: Ilikuwaje sasa mpaka akaondoka kabla hajawa sawa?
Tumaini: Nafikiri
ni uamuzi wake binafsi maana siku moja meneja wake (Babu Tale) alikuja
kumjulia hali, alipotaka kuondoka aling’ang’ania kuondoka naye. Sisi
pamoja na Tale tulimsihi sana kubaki lakini alikataa.
Risasi: Hali ilikuwaje kwa meneja wake wakati Chid anang’ang’ania juu ya jambo hilo?
Tumaini: Kiukweli
hakuwa akitaka aondoke maana mara kwa mara alikuwa anamsihi kuwa
mvumilivu ili amalize angalau miezi mitatu na ampeleke kwenye shoo za
muziki ndani na nje ya nchi, lakini Chid hakujali hayo. Kwa hiyo siwezi
kusema alifurahia juu ya jambo hilo.
Risasi: Maisha yake ya kawaida yalikuwaje na wenzake?
Tumaini: Hayakuwa
mabaya sana japo alikuwa mzito kushiriki kwenye ishu za usafi na vitu
vingine. Muda mwingi alipenda kupumzika na kuandika mistari. Lakini kuna
kipindi alikuwa akijaribu kuhamasisha wenzake wagomee kitu fulani. Sisi
tulikuwa tunamchukulia kama mtu wa kawaida aliyekuwa anahitaji msaada
kutoka kwa viongozi.
Baada
ya mahojiano hayo, waandishi wetu waliamua kumtafuta Chid Benz,
alipopatikana alikataa kuzungumzia suala hilo huku akisisitiza kuwa
lolote kuhusu yeye atafutwe Babu Tale.
Alipopatikana,
Babu Tale alisema: “Sitaki kusikiliza wala kuzungumza lokote kuhusu
Chid, muda ukifika nitaongea ila kwa sasa niacheni tu.”
0 comments:
Post a Comment