Msanii Snura Mushi ambaye wimbo wake
wa Chura ulipigwa marufuku
Snura amewaonesha kile alichosema ni cheti.
Msanii Snura Mushi ambaye wimbo wake
wa Chura ulipigwa marufuku na serikali ya Tanzania jana ameomba radhi na
kuahidi kutekeleza maagizo ya serikali.
Wimbo huo ulipigwa
marufuku na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ambayo ilisema
"maudhui ya utengenezwaji wa video ya wimbo huo “haiendani na maadili ya
Mtanzania.”
Mamlaka hiyo ilisema kazi hiyo inadhalilisha tasnia ya muziki.
Serikali ilipiga marufuku maonyesho yote ya hadhara ya Snura hadi
pale atakapokamilisha usajili wa kazi zake za Sanaa katika Baraza la
Sanaa la Taifa (Basata).
Akizungumza na wanahabari akiwa ameandamana na
meneja wake, Snura amesema amechukua hatua na kusajiliwa rasmi kwa ajili
ya shughuli za kisanii.



0 comments:
Post a Comment