Stori:Boniphace Ngumije
KUNDI
la Muziki wa Bongo Fleva linaloundwa na wapendanao wawili, Aika na
Nahreel ‘Navy Kenzo’ limefunguka kuwa moja ya mipango yake ya kikazi kwa
sasa ni kuhakikisha linashindana kibiashara na mkali wa muziki nchini
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na ikiwezekana hata kumshinda kupitia
lebo yao ya The Industry.
Akichonga
na gazeti hili, mama kijacho Aika alisema kuwa anachokifanya Diamond
kupitia lebo yake ya Wasafi, kukuza wasanii ni kitu kizuri lakini hata
hivyo kwa upande wao kutokana na aina ya wasanii walionao kwenye lebo
yao akiwemo Roseline Mohagachi ‘Seline’ aliyetoa wimbo mpya uitwao Njoo
wana imani watampita Diamond.
“Tumejipanga,
ukiangalia aina ya wasanii tulionao na namna wanavyoufahamu muziki
utakubali kuwa tunasonga mbele, ukweli ni kwamba Diamond asipoangalia
tutamkalisha chini,” alisema Aika.
0 comments:
Post a Comment