Ndege ya Shirika la EgyptAir iliyoaanguka baharini ikiwa na watu 69 leo.
Ndugu na jamaa wa abiria waliokuwa kwenye ndege hiyo wakiwa na simanzi.
Waziri Mkuu wa Misri, Sherif Ismail akiongea na wanahabari.
Rais
wa Ufaransa, Francois Hollande amethibitisha kuwa Ndege ya Shirika la
EgyptAir iliyotoweka kwenye rada ikiwa na watu 69 imeanguka kwenye
Bahari ya Mediterranean.
Hata hivyo Rais huyo amesema bado ni mapema kusema kwa ufasaha kabisa nini kiliisibu ndege hiyo yenye nambari MS804.
“Taarifa
tulizokusanya kufikia sasa, mawaziri, maofisa wa serikali na, bila
shaka, maofisa wa Misri, zinathibitisha, kwa huzuni, kwamba ndege
ilianguka. Ilitokomea.”
Rais
Hollande ameahidi kwamba serikali yake itatoa msaada unaohitajika na
maofisa wa Ugiriki na Misri wanaoendelea na juhudi za kuisaka ndege
hiyo.
Ofisi ya mwendesha mashtaka wa Paris nayo imesema imeanzisha uchunguzi kuhusu kutoweka kwa ndege hiyo iliyokuwa imepaa kutoka uwanja wa ndege wa Charles de Gaulle, Paris ikiwa na raia 15 wa Ufaransa.
Ofisi ya mwendesha mashtaka wa Paris nayo imesema imeanzisha uchunguzi kuhusu kutoweka kwa ndege hiyo iliyokuwa imepaa kutoka uwanja wa ndege wa Charles de Gaulle, Paris ikiwa na raia 15 wa Ufaransa.
Ndege
hiyo pia ilikuwa na raia 30 wa Misri, raia 2 wa Iraq na raia mmoja
mmoja kutoka Uingereza, Canada, Ubelgiji, Kuwait, Saudi Arabia, Algeria,
Sudan, Chad na Ureno.
Waziri Mkuu wa Misri Sherif Ismail amewaambia wanahabari kwamba juhudi za kuitafuta ndege hiyo bado zinaendelea.
Maofisa wa Misri na Ugiriki wanatumia ndege na meli kuitafuta ndege hiyo katika bahari ya Mediterranean.
0 comments:
Post a Comment