Akizungumza
na wanahabari katika Ukumbi wa Habari Maelezo ulipo Posta jijini Dar,
Alhamisi iliyopita, Snura aliomba radhi kwa serikali na Watanzania wote
waliochefuliwa na wimbo huo huku akisisitiza kuwa hakuna wimbo uliomtesa
kama Chura.
“Naomba radhi Watanzania wenzangu, sitarudia. Lakini
hata hivyo muelewe tu huu wimbo wa Chura ulinitesa sana kuliko hata
Majanga na Nimevurugwa. Nisemwa sana na watu mbalimbali na kuniita mimi
mhuni niliyepitiliza kwa ajili ya Chura tu.
“Watu walifikiri mimi
nilikuwa na dhamira mbaya ya kupotosha jamii na hadi kufikia hatua ya
kunitamkia maneno mabaya. Hata hivyo nimejifunza mambo mengi sana
kutokana na Chura na ninaahidi kuwa balozi wa maadili kwa wasanii
wengine,” alisema Snura. Katika mkutano huo na waandishi wa habari,
Snura alifafanua kuwa wimbo huo ulisimamishwa na serikali kwa kukiuka
maadili sambamba na yeye kutojisajiri katika Baraza la Sanaa na Taifa
(Basata) lakini siku hiyohiyo (Mei 4) aliyosimamishwa, alikwenda
kusajili Basata na kukamilisha taratibu zote hivyo yupo huru kufanya
sanaa na ataurekebisha wimbo huo na ataendelea kuutumia.
0 comments:
Post a Comment