Wednesday, June 29, 2016

Leo Tarehe 29 Rais Magufuli anawapisha wakuu wa mikoa na wilaya asubuhi hii live from Azam two na TBC1.


Rais Magufuli:
Gondwe ninajua unatangaza,sasa utakwenda kutangaza maendeleo unakokwenda,ufanye kama unatangaza tangaza tu.

Rais Magufuli:
Mchakato wa kuwapata Ma-DC haukuwa rahisi, ilibidi tutizame historia ya kila mmoja wao.

Rais Magufuli:
Kuna mabadiliko madogo tuliyoyafanya kutokana na jina lilikosewa, kwa hiyo aliyestahili tumeshamuweka.

Rais Magufuli:
Ningeweza nikataja majina yote mliopo hapa mpaka yule aliyepigwa fimbo na mtani wangu, karibu kila jina nalifahamu na sifa yake.

Rais Magufuli:
Mna mamlaka makubwa ya kumuweka mtu Mahabusu ila msiende tu kuonea watu.

Rais Magufuli:
Mnaweza kufikiri tumewachagua sisi lakini inawezekana Mungu ametutumia sisi kuwachagua ninyi.

Rais Magufuli:
Nilikuwa namuona DC wa Iringa anabeba watoto wakamsema sana, na mimi nikasema abaki hapa hapa

Rais Magufuli:
Nilitegemea sana baada ya kuwateua, nilitegemea labda mngekuja robo tu, ninawashukuru sana kwa kuja.

Rais Magufuli:
Watanzania wengi tumezoea kulalamika, tunapenda tu kupewa, hatutaki kufanya kazi.

Rais Magufuli:
Ni matumaini yangu hamtaniangusha, hata sura zenu zinaonyesha ni wachapa kazi, nendeni mkachape kazi.

Rais Magufuli:
Nyinyi wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya mna mamlaka hata ya kuweka watu mahabusu, ila msiende kuonea watu.

Rais Magufuli: Mkasimamie yale tuliyowaahidi sisi wana CCM, mkayatekeleze kwa nguvu zote
Rais Magufuli:
Watanzania wengi wana changamoto nyingi, nina imani hamtaiangusha serikali hii.

Rais Magufuli:
Nataka niseme ukweli, wale ma-DC tuliowaacha hawakufikia vigezo

Mchakato wa kuwapata ma-DC ulikuwa mgumu, ilibidi tuangalie historia ya kila mmoja, tuliangalia mambo mengi sana.

Rais Magufuli anazungumza kwenye sherehe za kuwaapisha kiapo cha uadilifu wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa wapya.

0 comments:

Post a Comment