Na Mwandishi Wetu, UWAZI
DAR
ES SALAAM: Mwezi Mtukufu wa Ramadhan umewadia na leo ni Chungu cha
Kwanza, Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Musa Salim amesema
kuna mambo matatu anayoyachukia au kumkera kwenye kipindi hiki.
Akizungumza
kupitia runinga moja jijini Dar es Salaam, Ijumaa iliyopita, shehe huyo
alisema kuwa, mara nyingi Ramadhan inapoingia, kuna baadhi ya Waislam
hufanya maasi wakisema ya mwishomwisho na kuyaita vunja jungu jambo
ambalo ni kinyume na Kurani.
Alisema: “Kwa kweli kuna mambo matatu huwa siyapendi kabisa wakati wa kukaribia mfungo wa ndani ya mfungo wenyewe.
“Kwanza
ni wale watu wanaofanya maasi halafu wanasema wanavunja jungu ili
kuingia kwenye mfungo. Pia, kuna wale wanaojisingizia maradhi wakati wa
Mwezi Mtukufu wa Ramadhan ili wasifunge. Hii si sawa hata kidogo.
“Lakini
jambo la tatu ni wale wanaohamia nchi nyingine. Kuna watu wakati wa
kufunga wanahamia kwenye nchi nyingine ili kukwepa funga. Haya ni mambo
matatu ambayo yananikera sana.”
Kutoka Dawati la Uwazi
0 comments:
Post a Comment