Tuesday, June 7, 2016

Pele kupiga mnada medali zake zote 


Nyota wa soka kutoka Brazil, Pele, ameamua kupiga mnada medali zote alizoshinda na vitu vingine vyenye dhamani alivyopata wakati alipokuwa mchezaji nguli duniani .



Mnada huo utakaodumu muda wa siku tatu, unaanza leo mjini London Mnada huo utakaodumu muda wa siku tatu, unaanza leo mjini London na unatarajiwa kukusanya mamilioni ya pesa.

Baadhi ya medali za Pele zitakazouzwa leo mjini London Wataalamu wanasema huenda mnada huo ukawa ndio mkubwa zaidi wa vifaa vya michezo kuwahi kufanyika.

Medali zote alizoshinda wakati wa kombe la dunia pia zitauzwa Medali zote alizoshinda wakati wa kombe la dunia pia zitauzwa wakati wa mnada huo.

Pele ambaye alianza kuchezea Brazil mika 60 iliyopita anasalia kuwa mfungaji bora zaidi wa mabao nchini humo.

Source: BBC Swahili

0 comments:

Post a Comment