NA RICHARD BUKOS
UNAMKUMBUKA
yule mwanadada ambaye umaarufu wake kwa kiwango kikubwa umetokana na
kupiga picha za nusu utupu? Huyu ni Faiza Ally na habari njema ni
kwamba, sasa ameamua kumrudia Mungu wake kwani amehisi alikuwa anapotea.
Faiza
aliliambia Ijumaa kuwa, watu wamekuwa wakimjua kwa staili yake ya kuvaa
kihasara lakini sasa hivi ameamua kuswali swala tano.
Akizungumza
na paparazi wetu maeneo ya Magomeni Mikumi jijini Dar kulikokuwa na dua
ya kumuombea Msanii wa Filamu, Salim Ahmed ‘Gabo’, Faiza alisema:
“Unajua Mungu ndiyo kila kitu, huwa tunajisahau tu lakini ukizinduka ni
vyema ukamrudia, kwa hiyo kwa sasa nitakuwa navaa hivi.”
0 comments:
Post a Comment