NA GLADNESS MALLYA
WAKATI
waumini wa Dini ya Kiislamu wakiwa ndani ya swaumu, staa wa filamu
Bongo, Tiko Hassan amefunguka kuwa na yeye yumo na ameamua kufunga kwa
sababu mbili za msingi. Akipiga stori na Ijumaa, Tiko alisema licha ya
kwamba kufunga ni nguzo muhimu ya Uislam lakini sambamba na hilo
anakitumia kipindi hiki kumuomba Mungu amjalie apate mume na afanye
vizuri kwenye fani yake.
“Namshukuru
Mungu kwa kunifikisha kipindi hiki, niseme tu wazi kwamba safari hii
nafunga nikinuia kabisa kuwa Mungu anijalie nipate mume maana nimechoka
kuishi maisha ya kipweke.
“Pili,
namuomba Mungu anijaalie katika fani yangu, kurwogana kumekuwa kwingi,
watu hawapendani, Mungu aniepushe na shari,” alisema Tiko.
0 comments:
Post a Comment