Mkuu wa Mkoa wa Mbeya amewataka wakuu wa wilaya zote mkoani Mbeya kusitisha mabaraza ya biashara kujadili fursa zilizopo katika wilaya zao na vikwazo mbalimbali vinavyowakabili wafanyabiashara katika wilaya zao
Hayo ameyasema Leo wakati akifungua kikao cha baraza la biashara ya mkoa wa Mbeya kujadili fursa za uwekezaji, biashara na changamoto zinawazowakabili wafanyabiashara na viwanda mkoani Mbeya
Amewataka watendaji ndani ya serikali j kuacha urasimu na rushwa katika utoaji wa leseni, ardhi, hati na vibali mbalimbali pale wafanyabiashara wanapokuwa wametimiza vigezo
Serikali haifanyi biashara na inategemea kodi ili kuendesha serikali na kutekeleza mipango ya maendeleo hivyo ni jukumu la serikali kujenga mazingira rafiki ya kuaminiana na wafanyabiashara katika kuongeza mapato ya serikali
Urasimu na rushwa vinakatisha tamaa wawekezaji na wafanyabiashara hivyo ni vema mambo haya yakakomeshwa kabisa ni rai yangu kuwa mabaraza haya yakiimarika ndiyo jukwaa ka serikali kukutana na wafanyabiashara na kusikiliza kero zinazowakabili wafanyabiashara na wawekezaji
Amezitaka wilaya kuibua fursa na kuzitangaza kwa ajili ya uwekezaji wenye tija katika wilaya zao










0 comments:
Post a Comment