Msanii wa muziki, Linah Sanga amesema mapenzi ni moja kati ya vitu ambavyo vimeathiri muziki wake.
Linah alisema hatua ya kuwatangaza wapenzi wake ni moja ya kitu ambavyo vimefanya mashabiki wake kufuatia maisha yake binafsi kuliko muziki wake.
“Kwa sasa hivi sitaki tena kuweka mbele maswala ya mahusiano yangu kuliko kazi, sasa hivi nataka watu wajue kazi zangu zaidi kuliko maisha yangu ya ndani,” alisema Linah.
Aliongeza,“Kuweka wazi mahusiano yangu kumeathiri muziki wangu kwa kiasi fulani, yaani watu wanapenda kusikiliza umbea umbea kuliko kusikiliza kazi zangu, hizi ni dalili mbaya kwangu, sasa hivi siweki tena maswala ya mahusiano yangu wazi,”
Muimbaji huyo alikuwa ni miongoni mwa wasanii wa muziki ambao wanapenda kuweka wazi mahusiano yao na kuonyesha jinsi wanavyokula bata.
0 comments:
Post a Comment