STAA
wa muziki Bongo, Snura Mushi ameibuka na kumkabidhi Makamu wa Rais,
Samia Suluhu jipu la wanaume wanaowakataa watoto wao na kuwaachia
wanawake mzigo wa kulea peke yao.
Akizungumza na Risasi Mchanganyiko,
Snura alisema siku hizi wimbi la wanaume kuwakataa watoto wao ni kubwa
sana hivyo tatizo hilo ni sawa na majipu mengine, anamuomba mama Samia
alitumbue.
“Namuomba
mama Samia kwa sababu ni mwanamke mwenzetu atusaidie kulitumbua hili
jipu maana ni kubwa sana yaani tena ni tambazi kabisa, kama rais
anavyowatumbua watu naye atumbue hili maana wanawake tumechoka.
“Nina
watoto wawili lakini baba zao wamenisusia, wa kwanza alimkataa tangu
nikiwa na mimba ya wiki mbili mpaka sasa nalea mwenyewe, huyu mwingine
hajawahi kutoa chochote tangu mwanaye huyu azaliwe kitu ambacho
kinaumiza sana,” alisema Snura.
Aliendelea
kusema kuwa baada ya mama Samia kutumbua hilo jipu anaomba serikali
iweke sheria ya kwamba kila kituo cha polisi kiwe kinapokea malalamiko
ya wanawake wanaosusiwa watoto au mimba ili shtaka linapokwenda
waandikishane na baada ya mtoto kuzaliwa ikigundulika mtoto ni wa
mwanaume husika alipishwe fidia.
“Pia
kipimo cha DNA kiwepo katika hospitali mbalimbali ili iwe rahisi kupima
kwa wale wanaume wanaokataa kwamba watoto siyo wao, sheria hizi
zikiwekwa zitasaidia kutokomeza tatizo hilo la watoto kukataliwa na baba
zao,” alisema Snura.
Jitihada
za kuzungumza na Waziri wa Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na
Watoto, Ummy Mwalimu kujua ameipokeaje changamoto hiyo, hazikuzaa
matunda kufuatia simu yake kutopatikana hewani.
Snura
ni mama wa watoto wawili kila mmoja na baba yake ambapo anawalea
mwenyewe huku akikiri kwamba huwa anawaeleza wanaye hao jinsi baba zao
walivyowakataa ili baadaye kusije kutokea mvutano wa kimasilahi pindi
watakapofanikiwa.
0 comments:
Post a Comment