Na Gregory Nyankaira, RISASI MCHANGANYIKO
MARA:
Hali mbaya! Wanandoa Said Somba (48) na Kadogo Ehijo (47), wakazi wa
Kitongoji cha Rugala, Kijiji cha Mazami, Kata ya Bukabwa wilayani
Butiama mkoani hapa wameuawa kwa kuchinjwa shingo na watu wasiojulikana,
Risasi Jumatano lina kila kitu.
Diwani
wa Kata ya Bukabwa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kitongoji cha Rugala,
Jonas Maswe aliliambia gazeti hili kuwa, tukio hilo lilijiri usiku wa
Mei 25, mwaka huu ambapo watu hao wakiwa na mapanga walivamia nyumbani
kwa Somba akiwa amelala na mkewe na kuwachinja.
Alisema
wakati wanachinjwa, wanandoa hao hawakupiga kelele na baada ya ukatili
huo wauaji hao waliifunika miili yao kitandani kisha wakatokomea
kusikojulikana.
Alisema mauaji hayo yalifanyika kimyakimya kwani hata watoto wa marehemu waliokuwa wamelala nyumba ya pili hawakusikia lolote.
“Asubuhi
ya saa 1 mtoto mmoja wa marehemu aliamka, akaenda kuwaamsha wazazi
wake ili wamfungulie mlango ajiandae kwenda shuleni.
“Mtoto
huyo aliwaita wazazi wake mara kadhaa bila majibu hivyo aliusukuma
mlango ambao ulikuwa umeegeshwa tu, akaingia ndani ya nyumba hiyo na
alipoingia chumba cha wazazi wake aliwaona wamelala wakiwa wamejifunika
shuka.
“Aliwasalimia
wakawa kimya, aliwashika na kukutana na dimbwi la damu, akawaona
wazazi wake wamefariki dunia huku wakiwa na majeraha makubwa shingoni.
“Yule mtoto alipiga kelele zilizowaita majirani nyumbani na kushuhudia unyama waliotendewa wanandoa hao,” alisema Maswe.
Mtoto
mkubwa wa marehemu hao, Amos Said (26) alisema kwamba, licha ya kuwepo
mifugo mingi nyumbani hapo kama vile ng’ombe na mbuzi, lakini wauaji
hao hawakuchukua mfugo hata mmoja.
Katibu
wa Tarafa ya Makongoro, Khamis Waryoba, alilaani kitendo hicho na kuapa
kusaidiana na Jeshi la Polisi Wilaya ya Butiama kuwasaka watu
waliohusika katika unyama huo.
Polisi
wilayani Butiama imethibitisha kuwepo kwa mauaji hayo na kusema
kuwa, wanaendelea na msako mkali wa kuwabaini waliohusika.
Akizungumzia
mauaji yanayoendelea, Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Musa,
alikemea hali hiyo, akiwataka Watanzania kumuomba Mungu aepushe roho
hizo za mauaji kwani hali siyo nzuri.
“Jamii
lazima imuogope Mungu, pia kwa kushirikiana na vyombo vya usalama
iwafichue wahalifu wanaotekeleza mauaji haya huku na sisi viongozi wa
dini tukiendelea kuwaombea ili waachane na roho mbaya walizonazo kwani
mambo kama haya hatujayazoea, tumekuwa tukiyaona kwenye nchi za
wenzetu,” alisema kiongozi huyo, akiungwa mkono na mchungaji wa kanisa
moja la kiroho lililopo Madale, Koplo Jacob.
“Siyo
jambo la kujivunia sana kuwa na jamii isiyoogopa mauaji, kila siku
unaposikia watu wanauana ni hatari kwa taifa, sala maalum inahitajika
ili kuwakomboa watu kifikra,” alisema.
Miili ya marehemu hao, ilizikwa Mei 26, mwaka huu, kwenye makaburi ya nyumbani kwao.
Bwana alitoa na Bwana ametwaa, jina lake libarikiwe. Amina.
0 comments:
Post a Comment