Tuesday, June 7, 2016

Na Mwandishi Wetu:- Juzi Blogu ya Wananchi ilimfuata The King Of All Bongo Social Media Network na kumkuta shambani kwake akiwa na Mrembo mmoja kwa jina Tully kutoka Mbeya, Blogu ya Wananchi tulimuuliza swali moja tu kwamba ana nini cha kujibu kuhusu mashambulizi mazito ya Mama wa Watoto wake 2 kwa kushirkiana na Mange? Mashambulizi ambayo yameiacha Dunia nzima kwenye mshangao mkubwa kutokana na ukweli kwamba Mange pia ni mtoto wa Kufikia wa Dada wa damu wa Le Mutuz Nation, The King akiongea kwa tabasamu alijibu ifuatavyo:- "Well, Neema aliamua kuvunja Ndoa Miaka 6 iliyopita, akadai na akabaki na watoto kama Sheria inavyosema, baadaye akaja na watoto Tanzania na kukataza nisiongee nao, now yote haya mimi sijawahi kuwa na tatizo nayo isipokuwa nimekuwa mtu wa kumkubalia kila anacholilia. Nilipo ondoka tu USA kurudi Tanzania akaanza kumfuatilia rafiki yangu wa karibu sana Msichana mmoja anayeishi South Africa akaanza kumpelekea sumu nyingi sana ili yule dada asishirkiane na mimi lakini yule dada akawa ananipa text zake zote, nikamuomba Dada yake Neema amuombe aniache kwa sababu sijamkosea kitu zaidi ya kuheshimu maamuzi yake yote. Majuzi akaamua kuanza kushirikiana na Mange mpaka kumpa copy ya Passport yangu na vitambulisho vingine ambavyo alifanikiwa kubaki navyo huko nyuma, na kibaya sana akadai kwamba Nyumba yangu na Shamba ni yake yeye. Now unajua mimi nimesomea Criminology & Policie Science kwa hiyo kwenye maneno mengi ya Mange nilikuwa natafuta hoja ya msingi inayomsumbua my ex nikagundua ana matatizo Mawili tu nayo ni Mimi na mylife style hasa ya Mabebezz na pili anaitaka sana Nyumba na Shamba so nimeamua kwamba hilo la lifestyle yangu ataendelea kupata majibu kwenye picha zangu za Social Media, kuhusu Nyumba na Shamba ni kwamba nilikuwa ninatafakari kwa muda mrefu sana nini cha kufanya nalo. Kwanza nilimuomba Mama yangu mzazi ahamie pale kutoka Tunduma, lakini hakutaka kabisa na mimi sina mpango kabisa wa kuhamia kule na Watoto wangu ni Wamarekani haitakuja kutokea kwamba watahamia Tanzania kwa hiyo nikawa nafikiria sana kumpa yeye lakini kwa haya aliyoyafanya nimeamua tena bila kufikiria mara mbili kuiuza na kuchana na Ukonga kabisa maana ile nyumba na shamba vipo karibu sana na kwao yeye na familia yake kwa hiyo kwa matatizo yote haya ninawezaje hata kwenda kuishi kule haitawezekana. Nikafikiria sana kumpa Mchumba wangu wa sasa lakini nikajua kwamba yatakuwa ni yale yale tu vita so nimeamua kuiuza. Ninataka kuweka nguvu zangu zote sasa kwenye Nyumba yangu ya Mbweni ambayo bado haijaisha, ingawa sina uhakika kama kuna siku nitakuja kuhama mjini nilipo sasa maana Miaka 30 ya kuishi Majuu ninapenda sana kuishi kwenye Apartment zaidi. Otherwise, ninamuombea sana kwa Mungu Neema maana amevurugika sana kichwani anayoyafanya yananishangaza sana kwa mtu aliyelilia sana kuvunja Ndoa, inaelekea hakujua kwamba ....Asiyefunfwa na Wazazi hufunzwa na Dunia, sasa dunia inamfunza maana ni mambo ya ajabu kwenda kwenye social Media na kuanza kumtukana Baba wa Watoto wako mwenyewe inashangaza sana hahahahahaha unajua Wasawahili wanasema ukiona panafuka moshi ujue kuna moto chini na ukiona mtumzima anaanza kwenda Social Media kumtukana Baba wa watoto wake ujue kwamba kuna mamuimivu mazito yanamtesa kuhusiana na Maisha mapya ya Baba watoto wake. I mean mtu anaishi USA ambako Wabongo wengi hapa nyumbani wanaombea kwenda kuishi leo unaishi USA unakuwa kama upo Bongo tu hahahaha inachekesha sana, lakini haina neno mimi huwa simchokozi mtu in my life ila ukinichokoza tu nitakujibu kwa lugha yako mwenyewe unayoielewa vizuri na pia nitaamua mimi kumaliza Vita kwa wakati wangu na kwa my terms. Na kuhusu Mange kuwa na uhusiano na ndugu yangu wa Damu hilo bado sijaliangalia ingawa nimeliona hata hilo nitalipatia jawabu pia"






0 comments:

Post a Comment