Kitendo
cha msanii wa filamu Bongo, Bond Suleiman kutumia usafiri wa bodaboda
kutoka Dar hadi Shinyanga kuwahi kumuuguza baba yake mzazi kimemponza.Akipiga stori na Za Motomoto News, Bond
alisema baada ya kufika kwao kwa kutumia usafiri huo licha ya baba yake
kuwa hoi,
alimjia juu na kumkanya asirudie tena kwani alitoka Dar saa
sita usiku na kufika saa 12 jioni ya kesho yake jambo ambalo ni hatari.
“Siyo
baba tu aliyekasirika hata majirani hawakupendezwa, sitasafiri tena na
chombo hiki umbali mrefu, nilifanya hivyo kwa sababu huku kijijini
usafiri ni wa shida mno na nilitaka kumuwahi baba yangu,” alisema Bond.
0 comments:
Post a Comment