Issa Mnally na Elvan Stambuli, UWAZI
Mtanzania
aitwaye Juma (jina lake la pili tunalihifadhi kwa sababu maalum)
anayedaiwa kumuweka rehani ughaibuni Mbongo mwenzake Adam Akida
Mwinyimkuu, mkazi wa Magomeni Mapipa jijini Dar es Salaam ambaye
ametekwa na kushikiliwa na watu wanaoaminika kuwa ni ‘Wazungu wa Unga’ ,
amekamatwa na polisi jijini Dar.
Uchunguzi
wa kina uliofanywa na waandishi wetu wiki iliyopita umebaini kuwa, Juma
alikamatwa na polisi mwishoni mwa wiki iliyopita Tegeta na anahojiwa
kuhusiana na kutuhumiwa kumuweka dhamana kijana Adam kisha kumtelekeza
ughaibuni huku ikidaiwa kuwa yeye alikuja na shehena ya unga.
Habari
zinasema ili Adamu awe huru, Juma anatakiwa kupeleka fedha shilingi
trilioni moja ambazo ni gharama ya unga aliopewa, huku akimfanya
mwenzake huyo kuwa ‘bond’ ya mzigo huo haramu.
“Fedha
anazodaiwa Juma ni nyingi ni shilingi trilioni moja. Ni kwamba mzigo
wenyewe (unga) hakufanikiwa kuuza kwani alikamatwa na askari
wakamnyang’anya na sasa sijui atafanya nini ili kumuokoa mwenzake aliye
ughaibuni,” kilisema chanzo chetu.
Habari
zaidi zinasema kuwa licha ya Juma kuwa korokoroni, baba wa Adamu mzee
Akida Mwinyimkuu naye alishikiliwa kwa muda na polisi katikati ya wiki
iliyopita lakini hakuwa na msaada wowote kwa vyombo vya dola.
“Mzee
Akida alikamatwa na polisi lakini badala ya kusaidia akawa anapotosha
ukweli. Yeye aliwaambia polisi kuwa mtoto wake Adam hakwenda Pakistani
bali alikwenda Afrika Kusini na ndivyo anavyojua. Alipooneshwa video ya
mwanaye akiwa chini ya ulinzi, alishangaa na hakuwa na la kusema,”
kilisema chanzo chetu.
Kamanda
wa Polisi wa Kikosi cha Kuzuia na Kupambana na Madawa ya Kulevya
Tanzania, SACP Mihayo Msikhela (pichani) alipoulizwa na gazeti hili
kuhusu kukamatwa kwa mzee Akida na Juma hakukiri wala kukataa.
“Unajua
hili jambo bado lipo kwenye uchunguzi, hatuwezi kusema chochote hadi
tumalize uchunguzi wetu lakini wote wanaotuhumiwa tunawasaka na
tukiwakamata tutawahoji. Tukimaliza upelelezi wetu tutatoa taarifa kwa
umma,” alisema kamanda huyo.
0 comments:
Post a Comment