Monday, July 4, 2016

 Mkurugenzi Mtendaji wa DSTV Tanzania Mr. Maharage Chande leo akiongoza wafanyakazi wa DSTV kukabidhi misaada ya kusaidia kuendesha Kituo cha Watoto wa Yatima cha El Medina Tandale. DSTV Tanzania imekuwa mfadhili mkubwa wa Kituo hiki ambacho imekuwa ikitoa misaada mara mbili kwa Mwaka toka Mwaka 2009 mpaka leo. Akizungumza leo MD Chande alisema kwamba DSTV Tanzania itaendeleza tabia hiyo ya kukisaidia kituo hicho ili kukipa unafuu wa gharama za kutunza watoto hao ambao alisema ni muhimu sana kwa Taifa.
Mr. Maharage Chande Mkurugenzi Mtenndaji wa DSTV Tanzania kati kati akiongea na Mkuu Muendeshaji wa Kituo cha Watoto wa Yatima El Medina Mama Kuluthumu, baada ya kumkabidhi Misaada mbali mbali leo kwenye kituo hicho Tandale na kulia ni Le Mutuz Nation.


Wafanyakazi wa DSTV Wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Mr. Chande Maharage wakipiga picha ya pamoja na watoto hao wa Yatima leo baada ya kukabidhi misaada hiyo leo.





Waoto hao wa Yatima kituo cha El Medina wakiangalia baadhi ya bidhaa za misaada waliyopewa na DSTV Tanzania leo.













0 comments:

Post a Comment