Wednesday, July 27, 2016


KATIKA kile kinachoonyesha UKAWA kuwa wameishiwa na hoja,ni pamoja na kuibuka na wazo la kile wanachpokiita kupinga udikteta ambao wazi wamedai kuwa unafanya na Rais JPM.


Lakini hiini tofauti na matamko yao katika miaka kumi iliyopita ambapo kila walipokuwa wanapata nafasi ya kuhubiri majukwaani walikuwa wanadai kuwa ili nchi iendele wanahitaji kupata Rais Dikteta ambaye ataweza kuisimamia nchi hii vizuri.

Baada ya Rais JPM kuingia madarkani siku za mwanzo walikuwa wanaema kuwa anatekeleza ilani ya UKAWA na CHADEMA kwa ujumla,kadri siku zilivyokuwa zinakwenda mbele wakaanaza kulia kutokana na jinsi Rais anafanya kazi zake ambapo walianza kudai kuwa anayofanya Rais tena si Ilani yao.

Wakaona haifai wakaanza kula matapishi yao wenyewe kwa kumwita Rais JPM eti ni Dikteta,wakati huo wanasahau kuwa ndio waliokuwa wanalia Nchi iongozwe na Rais Dikteta miaka 10 iliyopita.

0 comments:

Post a Comment