Mkuu wa Mkoa amewaomba wananchi na wafanyabiashara kutumia siku ya kupatwa kwa jua septemba 1 kama Fursa
Kikao kwa kauli moja kimeridhia mapendekezo YA baraza la madiwani halmashauri mama ya Chunya juu YA mgawanyo wa Mali , watumishi na madeni

Mkuu wa Mkoa amezitaka halmashauri hizo mbili kuendeleza umoja na ushirikiano na si kwamba baada ya uamuzi huo wasitishe ushirikiano na kubadilishana uzoefu
Aidha amewahakikishia wabunge na madiwani kuwa serikali kwa ngazi zote itawapa ushirikiano bila kujali itikadi za Siasa
Amewaomba wananchi wa Mbeya hususani wafanyabiashara kutumia ujio wa watalii toka kila kona ya dunia kama fursa kufuatia tukio la kupatwa kwa jua tarehe 1 septemba mwaka huu wilaya ya wangingombe na Mbarali maeneo hayo yamethibitika ndiyo yatakayoonyesha kwa asilimilia 99 kupatwa kwa jua

Serikali ya Mkoa itahakikisha usalama kwa wote watakafika kushuhudia tukio hilo tarehe 1 septemba kuanzia saa 1 asub mpaka saa nne asubuhi



0 comments:
Post a Comment