Sunday, July 10, 2016

Waziri mkuu wa zamani na aliyekuwa mgombea urais kupitia CHADEMA, na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Edward Ngoyai Lowassa alikuwa mgeni rasmi katika mkutano wa Umoja wa Mameya na Wenyeviti wa Halmshauri wa CHADEMA-Tanzania uliofanyika jijini Arusha na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa chama hicho.
Wakati alipokaribishwa kuzungumza katika mkutano huo Lowassa amekitaka chama hicho kuachana na uanaharakati na maandamano ya kila mara na badala yake kijipange kushika dola katika uchaguzi mkuu ujao 2020.
“Chama cha siasa kazi yake ni kukamata dola basi, hakuna kitu kingine duniani, vision ya chama cha siasa ni wanasiasa kukamata dola, mnapokaa hapa mjiandae kukamata dola na sio kitu kingine, acha habari ya maandamano, maandamano ni process”-alisema Lowassa
Katika hatua nyingine, Lowassa amewataka vongozi hao kuhakikisha wanafanyakazi ya kuwatumikia wananchi na kuacha kupigania tenda za halmashauri au ugomvi wa viwanja kila kukicha kwani ndiyo kazi ya madiwani wengi.Amewataka wafanye kazi kwa utofauti kwani wananchi wanategemea kuona vitu vya tofauti kutoka kwao.
Aidha, mameya na wenyeviti hao walilalamikia kodi za kila namna zilizopo ambazo zinakwamisha maendeleo kwani zinamnyonya yule mtu wa chini na kushindwa kujikwamua.

0 comments:

Post a Comment