Wamarekani Weusi waliouawa na polisi Marekani, Alton Sterling (kushoto) na Philando Castile (kulia) enzi za uhai wao.
Maandamano
ya Wamarekani Weusi nchini Marekani kupinga mauaji ya wenzao wawili
yamechukua sura mpya baada ya kuingia siku ya tano huku polisi wakiwa
katika tahadhari kubwa kutokana na kuwepo tetesi za mipango ya mauaji ya
polisi wengine.
Tahadhari hiyo imekuja ikiwa ni siku chache baada ya mauaji ya polisi watano katika Mji wa Dallas.
Waandamanaji
wenye hasira wameendelea kuandamana huko Baton Rouge, Louisiana, ambapo
mfanyabiashara wa mtaani Alton Sterling alikamatwa na kupigwa risasi na
polisi wawili Jumanne asubuhi.
Katika maeneo kadhaa nchini humo polisi wameendelea kuwakamata wananchi hao.
Waandamanaji
katika eneo la St Paul, Minnesota ambapo Mmarekani mwingine mweusi,
Philando Castile aliuawa na polisi mzungu waliwatupia fashifashi na mawe
polisi na kuwajeruhi watatu.
Sehemu
nyingine ambapo maandamano yanaendelea ni New York, San Francisco,
Denver, Florida, Pittsburgh, Philadelphia, Salt Lake City na Rhode
Island.
0 comments:
Post a Comment