Posted by Williammalecela.com on Tuesday, July 19, 2016
 |
"Leo
asubuhi nimemtembelea Muwekezaji Kijana Ndg John Chobo ambaye anamiliki
kiwanda cha kuchakata nyama katika eneo la Usagara mkoa wa Mwanza.
John amekuwa ni kijana ambaye alijua anataka nini na kuwa nani na
ameishi katika kutimiza ndoto zake na leo amefikia hatua ya kuwa na
uwekezaji wa zaidi ya Tsh 8 Bilioni na kuwa na mashine za kisasa katika
Afrika Mashariki.
Mpaka sasa ameshatoa elimu ya ufugaji wa kisasa kwa vijana zaidi ya 600 wa maeneo ya kanda ya Ziwa na mradi huu unategemea kuajiri zaidi ya watu 700.
Serikali inaunga mkono jitihada hizi za wawekezaji vijana na itaendelea
kuboresha mazingira ya uwekezaji ili vijana wengi zaidi washiriki
katika uchumi wa Taifa.
Inawezekana tukitimiza wajibu wetu"
|
0 comments:
Post a Comment