Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla leo ametembelea eneo la Pandahill kata ya Songwe mahali ambapo patachimbwa madini adimu aina ya Niobium ambayo hutumika kutengeneza Ndege na computer na mpaka sasa madini hayo huchimbwa bara la Amerika tu na kugundulika kwa madini hayo Tanzania utakuwa mgodi wa nne duniani na wa kwanza Afrika
Mkurugenzi wa kampuni ya Pandahil limited ndg Derick amesema imewachukua zaidi ya miaka 5 kufanya utafiti na kugundua uwepo wa madini hayo, taratibu zote za kisheria zimekamilika na kampuni hiyo itawekeza zaidi ya shilingi bilioni 500 katika mradi huo na mradi utatengeneza ajira watu 500 na mradi huo utaanza uzalishaji mapema mwaka 2018
Mkuu wa mkoa ameipongeza kampuni hiyo kwa ugunduzi na uwekezaji huo mkubwa na akawataka washirikiane na viongozi na wananchi kwa kila hatua ili kuweka wazi mradi huo kwa wananchi

Amewashukuru kwa mchango wa madawati 400 ambayo yatasambazwa kwa shule 7 zilizokuwa na upungufu wa madawati
Aidha amewataka wananchi na viongozi kutoa ushirikiano kwa kampuni hiyo ili wananchi wanaozunguka eneo hilo uzalishaji utakapoanza wafaidike na ajira, huduma za jamii na kodi mbalimbali kwa hslmashauri na serikali kuu



0 comments:
Post a Comment