Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla amezindua kivuko cha Kiteputepu kijiji cha Mbaka wilaya ya Rungwe baada wananchi hao kupata shida ya kuvuka na kuhatarisha maisha kwa kuvusha watoto kwenda Shule kwa kuogelea, kukosa huduma za jamiii hasa mto unapojaa Maji 
Tarehe 10 juni mhe Jenista Mhagama,Waziri ofisi ya waziri Mkuu kitengo cha maafa alifika kujionea changamoto hiyo na ofisi yake ilichangia shilingi milioni 10 na mnamo tarehe 16 juni Mkuu wa mkoa kwa kushirikiana na halmashauri alipatikana mkandarasi na alimpa wiki 2 amalize kazi na akahaidi terehe 8 julai( LEO) angekuja rasmi kuzindua kuvuko hicho na ahadi hiyo ameitimiza leo

Gharama ya ujenzi kivuko ni shilingi milioni 58 na kufuatia uzinduzi huo wakazi wapatao 700 wa kitongoji cha Kibundungulu wameanza kukitumia kivuko hicho kwa kupita kwa miguu na pikipiki

Amewataka kukitunza kivuko hicho kwani ujenzi wa daraja la kudumu unahitaji fedha nyingi zaidi ya bilioni 1.5 hivyo ni vema wakakitunza kivuko hicho kwasasa kwani kwa kiasi kikubwa kitapunguza tatizo la kuvuka na kwenda vijiji vingine

0 comments:
Post a Comment