‘In due time’ kwa maneno ya Seven Mosha, huenda Barakah Da Prince akaja kuungana na Alikiba kwenye roaster ya label ya Sony Music
Seven ambaye ni meneja wa Barakah kupitia kampuni ya Rockstar4000 alipost picha ya muimbaji huyo na kuandika maneno matatu tu yenye maana kubwa, ‘in due time’ akimaanisha kuwa muda ukifika.
Naye muimbaji huyo wa ‘Siwezi’ ameshare picha kadhaa kwenye Instagram akiwa kwenye makao makuu ya Sony Music tawi la Afrika jijini Johannesburg.
Kwenye picha moja wapo ameandika: Before leaving SA, I had a visit at the Sony offices for inspiration and kuelewa zaidi the music business. #ImUpToSomething #IamARockstar.”
Kwenye picha nyingine ya ukutani ya mfalme wa pop, Michael Jackson, Barakah ameandika: One of my biggest inspirations @michaeljackson nae alikuwa chini ya Sony Music International na hichi ndio chumba dedicated to him at Sony Music.”
Muimbaji huyo alikuwa nchini humo kushoot video pamoja na kuzunguka kwenye vituo mbalimbali vya redio na TV kwaajili ya interview.
0 comments:
Post a Comment