Thursday, July 28, 2016

 
Wananchi wapongeza wasema huu ni utaratibu wa aina yake
-Mkuu wa Mkoa asema utaratibu huu ni wa kudumu mpaka siku atakapifika ukumbini akute hakuna Mwananchi mwenye Kero- Kero Nyingi ni maeneo yanayohusu Ardhi, na lawama kwa mabaraza YA ardhi na jeshi la polisi 
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla leo ameendelea na utaratibu aliyojiwekea wa kusikiliza Kero za wananchi na kuzipatia ufumbuzi kila siku ya Alhamisi ya mwanzo wa mwezi na siku ya alhamis ya mwisho wa mwezi kama kawaida siku ya leo mamia ya wananchi wamejitokeza Mbele ya Mkuu wa Mkoa kuwasilisha kero zao
Mkuu wa Mkoa amewataka wakuu wa wilaya na watendaji wa ngazi zote kuwasikiliza wananchi na kutatua Kero zao" Kero Nyingi hapa ni za halmashauri, wakuu wa wilaya, wakurugenzi na wakuu wa idara tafadhalini hakuna jambo kubwa katika uongozi kama kuwa Karibu na unaowaongoza, kuwa msikivu na kushughulikia matatizo yao kwa umati huu ni dhahiri hamjatimiza majukumu yenu na kwa kuwa MaDc, ma Ded ni wapya sasa anzeni kazi hii kwa kasi "
Amekitaka jeshi la polisi kuharakisha upelelezi wa kesi na pia kuepuka vitendo vinavyolalamikiwa kwa baadhi ya askari kubambikizia wananchi kesi
Amehaidi kuendeleza utaratibu huu kwa muda wote mpaka siku atakapofika ukumbini akute hakuna Mwananchi aliyeleta Kero

0 comments:

Post a Comment