KIFO CHA NYANI MITI YOTE HUTELEZA!
Nimekuwa nikifuatia kwa makini sana sakata la Tundu Lissu na majigambo yake ya kupigania Demokrasia ya kuchora huku msanii huyu akimwita rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hii kuwa ni DIKTETA UCHWARA...
Pengine labda mimi ndio sielewi lakini kweli hivi kweli mtu anayepigania Demokrasia nje ambayo hata nyumbani kwake haipati ni Demokrasia gani haswa anayopigania yeye. Ndio yale ya Nyani haoni makalio yake ama kitu gani? Mnataka nini haswa Upinzani maana sijawaelewa kabisa..
Na iweje hawa viongozi wa Vyama wa Upinzani wameshindwa kabisa kujitazama wao katika kioo ama waulize wananchama wao ili wakajielewa kuwa wao wenyewe ni Madikteta toka nitoke! Hawakubali kukosolewa, Hawakubali ushindani, Hawakubali kuelekezwa maana wao na Kamati zao Kuu wanajua zaidi ya wanachama wote. wakishitka nchi watu hawa watanyanganya watu Urais maan ndani ya vyama tu kazi yao kubwa ni kufukuza mshindani utadhani dume la Punda..
Viongozi hawa wote na kwa vyama vyote ni Mayatollah - Ma Supreme Leaders, wengine wameongoza kwa miaka 15 hadi 20 pasipo kupingwa, iweje leo Tundu Lissu azungumzie Demokrasia ya Kitaifa ilhali hawezi kumnyooshea kidole Lowassa, Mbatia, Maalim Seif wala Mbowe! dhidi ya Utawala ambao wamepewa fursa walipogombea Ubunge japo hao hao ndio viongozi wa chama, wakaingia Bungeni wasivue kofia zao za Wenyeviti ama Makatibu wakuu wa vyama. Tena naweza sema wamevaa kofia zaidi ya mbili wakipokea mishahara na posho Kushoto na Kulia.
Hivi kweli Tundu Lissu, Unataka kuona jinsi gani wananchi walivyo nyuma ya Magufuli? Je, unataka kuziona hasira za wananchi watakapo chukua wao sheria wafanye maandamano nchi nzima kumuunga Mkono John Pombe Magufuli utabakia kaitka hali gani. Ni Demokrasia gani mnaoililia isiyohusiana na wananchi wenyewe..Tutakuamini vipi Tundu Lissu na busara zako ikiwa uliwahi kumsimanga Zitto Kabwe na kisha Slaa na kuyasema haya http://www.jamiiforums.com/…/tundu-lissu-dr-slaa-n…/page-61…
Leo umefikia kumwita JPM kuwa RAIS UCHWARA kwa sababu tu umefungiwa kungia Bungeni unazikosa Posho za vikao maisha yamekuwa magumu, Umekatwa ulimi wa kauli Bungeni kujitangaza na kubakia Msukule ama Kibogoyo unabwabwaja kana kwamba wananchi wanakuelewa. Mara unakurupuka ati Busara ni Bidhaa Adimu. Toka Lini BUSARA ikawa Bidhaa? katika kuelimika kwako kweli uliweza kuinunua BUSARA na soko gani hilo? na mbona hizo busara huna kaka. Ama kweli leo umeonyesha jinsi gani ulivyo ukisha vuliwa nguo.. Mdogoooo!
Upinzani kwa Ujumla, hayo madai yenu ya Demokrasia hayana Tija kwa wananchi hata kama Magufuli akiwapa yote, hakuna kitakacho badilisha Maisha ya Wananchi isipokuwa yenu Nyie na siasa zetu za Majitaka.Na inasemekana kinachowauma zaidi ni punguzo la mishahara yenu, Kodi msizotaka kulipa na sasa Maadili. Haya yanawagusa nyote Wabunge na Viongozi wa vyama vyote toka hiyo CCM hadi Upinzani chini ya huyo Godfather wenu, hivyo mmeunda FITNA dhidi ya JPM lakini mkumbuke wananchi wengi wapo nyuma yake..

0 comments:
Post a Comment