Tuesday, July 5, 2016


Tokea atangaze kuanza Tour ya kitalii nchini Hisania katika visiwa vya Ibiza au VIKISHENI kama anavyoiita mwenyewe,mkali wa track ya ACHIA BODY ,Ommy Dimpoz amejikuta katika wakati mgumu kwa mashabiki wake kutokana na picha anazopost katika ukurasa wake wa Instagram.

Katika kile kinachoonyesha kuwa kimewakera mashabiki wake,baadhi ya mashabiki walimshukia nyota huyo kwa tabia hiyo ya KUPONDA RAHA huku akifahamika vema kuwa ni Muislam na angepaswa atumie muda huo kuwa karibu na Mungu wake ikizingatiwa kuwa kipindi hiki ni kipindi cha mwezi mtukufu.

Mashabiki wengine walisema kuwa Dimpoz kutokana na matendo anayoyafanya staa huyo mwenye dimpozi na mwili uliojengeka vema,huenda vikamfanya afulie kimuziki.
A photo posted by Ommy Dimpoz (@ommydimpoz) on

Hata hivyo katika moja ya picha alizoweka staa huyo,alionekana akiwa anakula na rafiki zake kitendo ambacho pia kilizidisha munkari kwa mashabiki wake wengi

0 comments:

Post a Comment