Monday, July 18, 2016

 Meneja Bidhaa wa Dodoma Wine Warda Kimaro akiongea na wageni waalikwa wakati wa uzinduzi wa mvinyo mpya wa Dodoma Rose. Uzinduzi huo uliofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
 Mtaalam wa kutengeza mvinyo wa Dodoma Rose Erick Schlunz akiwaelezea wageni waalikwa sifa na ladha ya mvinyo huo mpya uliozinduliwa rasmi jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

 Meneja Bidhaa wa Dodoma Wine Warda Kimaro (kulia) akipita kugonganisha glasi na wageni mbalimbali waliohudhuria uzinduzi wa mvinyo mpya wa Dodoma Rose. Uzinduzi huo uliofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Cheers: Wageni waalikwa wakigonganisha glasi kufurahia uzinduzi wa mvinyo mpya wa Dodoma Rose. Uzinduzi huo uliofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Kampuni ya Tanzania Distilleries Limited (TDL) kupitia bidhaa yake ya Dodoma Wine mwishoni mwa wiki imezindua mvinyo mpya wenye rangi ya pinki uitwao “Dodoma Rose Wine.”
Akizungumza katika uzinduzi huo, Meneja Bidhaa wa Dodoma Wine, Warda Kimaro, alisema, pamoja na kuwapatia wateja wao mvinyo wenye ladha tofauti, Dodoma Rose pia inapanua wigo kwa wakulima mkoani Dodoma kuendelea kuwa na soko la uhakika hivyo kuwawezesha wananchi kiuchumi.
“Ujio wa bidhaa hii ya Dodoma Rose maana yake ni kuongeza mahitaji ya mali ghafi ya kutengenezea mvinyo”, alisema Kimaro. Dodoma Rose inapatikana Tanzania nzima katika ujazo wa 750 ml kwa bei ya rejareja ya Tshs 10,000
Kuzinduliwa kwa mvinyo wa Dodoma Rose kumeongeza idadi ya mivinyo ya jamii ya Dodoma kufika minne. Nyingine ni Dodoma Dry Red Wine, Dodoma Dry White Wine, Dodoma Natural Sweet Wine na sasa Dodoma Rose Wine. “Pamoja na kwamba Dodoma Wine hutengenezwa hapa hapa nchini lakini ina ubora wa hali ya juu unaokidhi kiwango cha kimataifa”, alisema Kimaro na kuogeza kuwa kauli mbiu ya Dodoma Rose wine ni onja ladha tofauti.
Alisema mbali na Dodoma kuwa mji mkuu wa nchi yetu; lakini pia umekuwa maarufu kwa kuzalisha mvinyo wa pili kwa ukubwa katika Afrika kusini mwa Sahara. “ndiyo maana ikaitwa Dodoma Wine kuonyesha mizizi yake na kutambua urithi wetu. Dodoma Wine ilizinduliwa 2010 Na inatengezwa kutoka kwa zabibu bora kabisa zinazolimwa na wakulima wetu wa Tanzania”, alisema.
Akiongea zaidi jinsi kampuni ya TDL inavyounga mkono wakulima wa zabibu, Mkurungenzi Mtendaji wa TDL Devis Deogratius alisema, ‘Wakulima wa zabibu walikuwa na hali ngumu hapo zamani lakini kupitia miradi tumeweza kuwainua wakulima sio tu kuwapa soko la uhakika pekee, lakini pia kwa kuwapa ujuzi wa kulima zabibu kupitia mtaalamu wetu wa kutengeneza kinywaji cha Dodoma Wine Erik Schlunz, ambaye leo tuko naye hapa’.
Mtengenezaji wa kinywaji cha Dodoma Wine Erik Schlunz alipata nafasi ya kuwatembeza wangeni waalikwa na kuwapa uzoefu wa kuonja mvinyo mbali mbali ya Dodoma Wine.
Devis alisema kuwa kampuni yake imejipanga kutangaza Dodoma Wine sehemu mbalimbali nchini na hasa kwenye baadhi ya sehemu za starehe na maduka makubwa (supermarket) ili kuwwaezesha wateja wao kutambua ni mvinyo ngani unaowafaa. Aliongezea kuwa uzinduzi huu wa Dodoma Rose Wine ni uthibitisho wa mafanikio yanayotokana na mvinyo wa Tanzania pamoja na wakulima wa zabibu. 

0 comments:

Post a Comment