Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla amezitaka halmashauri za mikoa 7 ya nyanda za juu kusini , washiriki, wananchi na wadau mbalimbali kuhakikisha maonyesho ya nanenane mwaka huu yatakuwa ya mfano hivyo amewataka kujipanga na kufanya maandalizi mazurii kuliko maonyesho ya kanda zingine
Hayo ameyasema leo jijini Mbeya katika kikao cha maandalizi ya maonyesho ya nanenane ya nyanda za juu kusini yanayojumuisha mikoa 7 ambayo ni Mbeya,iringa, Njombe, Songwe, Ruvuma,Rukwa na Katavi

Aidha amekieleza kikao hicho kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa maonyesho hayo tarehe 1 /8/2016 atakuwa Dr Charles Tizeba( Waziri wa kilimo, mifugo na uvuvi) na kilele cha maonyesho hayo itakuwa tarehe 8/8/2016 na mgeni rasmi atakuwa Waziri Mkuu wa jamhuri ya muungano Kassim Majaliwa( mb)

Hivyo amewaaomba washiriki, wadau na wananchi kujitokeza kwa wingi katika maonyesho hayo

0 comments:
Post a Comment