Stori: Issa Mnally
DAR
ES SALAAM: Baadhi ya viongozi wa dini nchini wanadaiwa kukwepa kodi kwa
kutumia taasisi zao za dini ambazo zimekuwa zikipata misamaha ya kodi
kwa kile kinachoelezwa kuwa vitu wanavyoviingiza ni mali ya kanisa,
misikiti au taasisi ya kidini, wakati baadhi yao hudanyanga, wanasakwa
na serikali kwa kosa la kukwepa kulipa kodi.Chanzo chetu cha
habari ndani ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru)
nchini zinasema kuwa viongozi hao wa kidini wamekuwa wakitumia mwanya
huo wa misamaha ya kodi
kujinufaisha wenyewe kwa kuingiza magari ya
kifahari ambayo huyatumia wenyewe au wafanyabiashara wazoefu wa kukwepa
kodi.Akizungumza na Wikienda, afisa mmoja wa Takukuru jijini Dar ambaye
aliomba hifadhi ya jina kwa kuwa siyo msemaji wa taasisi hiyo lakini
alikiri kwamba kuna baadhi ya viongozi wa dini wanasakwa kutokana na
madai ya kukwepa kodi kiujanja.“Wamekuwa wakiingiza vitu vingi tu
yakiwemo magari ya kifahari lakini hayatumiwi kwa shughuli za kidini
badala yake wamekuwa wakitumia wenyewe katika shughuli binafsi au
mengine yanaingizwa kwa jina la taasisi lakini utakuta ni mali zao au
wafanyabiashara nje ya taasisi zao,” alisema afisa huyo.Akaongeza:
“Nakumbuka kuna viongozi fulani wa kidini walikamatwa na kuhojiwa katika
ofisi zetu za Magomeni kwa kuingiza magari ya kifahari kumbe
waliwaingizia watu kupitia taasisi yao ya kidini na huku wenyewe
wakipanda daladala.”Alisema viongozi hao waliyatoa magari hayo bandarini
baada ya kupata msamaha wa kodi kupitia kwa mkuu wa wilaya lakini kuna
taarifa kwamba sasa yanatembelewa na watu wenye fedha, hivyo uchunguzi
wa suala hilo unaendelea.Askofu mmoja wa Kanisa la Ufunuo Tanzania, Paul
Bendera alikiri kusikia kuwa baadhi ya taasisi za kidini hutumia mali
zinazoingizwa kwa jina la taasisi hizo lakini hutumika kwa matunizi
binafsi na kuitaka serikali kuwachukulia hatua viongozi hao.
“Dini
zote zinajenga amani ya nchi na kazi za serikali ni kuhakikisha kila
mtu analipa kodi bila kujali dini au kabila. Serikali ichukue hatua za
kisheria dhidi ya viongozi wa kidini wanaofanya hivyo,” alisema askofu
huyo.
0 comments:
Post a Comment