NA IMELDA MTEMA,
WASTARA
Juma ambaye alikataa mahari ya shilingi milioni tano ya kijana Juma
Mbega ‘Masairo’, hivi karibuni walionekana laivu katika picha za pozi
tofauti walizopiga sehemu mbalimbali jijini Dar es Salaam.
Chanzo
kilichovujisha picha hizo, kinasema licha ya mahari hiyo kukataliwa,
lakini wawili hao hivi sasa ni kama kumbikumbi, kwani huonekana pamoja
kila wanapokwenda, tena wakitumia gari la muigizaji huyo.
Inadaiwa
kuwa wawili hao awali walikuwa wakiishi nyumba moja, enzi za uhai wa
marehemu mume wa Wastara, Juma Kilowoko ‘Sajuki’ ambaye alikuwa ni
rafiki yake, hivyo kijana huyo kuwa kama shemeji wa muigizaji huyo.
Gazeti
hili lilimtafuta Wastara, ambaye alikiri kuwa karibu na kijana huyo,
lakini akidai anafanya hivyo kwa vile ni kama shemeji yake ambaye
ameishi naye kwa muda mrefu.
Kwa
upande wake, Juma alisema Wastara ni mtu anayemsaidia katika mambo
mengi, lakini pia amemsogeza karibu ili kumfanya awe na furaha na
kutowapa watu nafasi ya kumchezea.“Sitaki kupinga kuwa Wastara ni mtu
muhimu sana kwangu, na sitaki kumpa nafasi mtu yeyote yule kumuumiza na
kumkosesha furaha kwa sababu najua aliyekuwa akimpatia ni kaka yangu tu
Sajuki,” alisema Juma.
0 comments:
Post a Comment