Posted by Williammalecela.com on Wednesday, August 24, 2016
 |
"Usiku
huu nimefika Mbande - Temeke,eneo lilipofanyika tukio baya la uhalifu
wa kutumia silaha ambapo watu/majambazi zaidi ya saba wakiwa na silaha
wamevamia eneo la Benki ya CRDB-Mbande
na kuua askari 4 waliokuwa
wakishuka kwenye gari tayari kwa kupokezana lindo. Pia wamejeruhi raia wa kawaida wawili,nimewajulia hali zao na wote wanaendelea vizuri.
Hatutaishia kulaani tu tukio hili na matukio mengine kama haya,natoa
rai kwa wahusika kujisalimisha.Vilevile wananchi na raia wema tunaomba
ushirikiano wenu katika vita hii ya kupambana na wahalifu hawa na
wanaotuzunguka kwenye maeneo yetu." |
0 comments:
Post a Comment